Swahili
Surah Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya count 19
إِذَا السَّمَاءُ انفَطَرَتْ
( 1 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 1 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 1](style/islamic/icons/mp3.png)
Mbingu itapo chanika,
وَإِذَا الْكَوَاكِبُ انتَثَرَتْ
( 2 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 2 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 2](style/islamic/icons/mp3.png)
Na nyota zitapo tawanyika,
وَإِذَا الْبِحَارُ فُجِّرَتْ
( 3 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 3 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 3](style/islamic/icons/mp3.png)
Na bahari zitakapo pasuliwa,
وَإِذَا الْقُبُورُ بُعْثِرَتْ
( 4 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 4 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 4](style/islamic/icons/mp3.png)
Na makaburi yatapo fukuliwa,
عَلِمَتْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ وَأَخَّرَتْ
( 5 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 5 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 5](style/islamic/icons/mp3.png)
Hapo kila nafsi itajua ilicho tanguliza, na ilicho bakisha nyuma.
يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ مَا غَرَّكَ بِرَبِّكَ الْكَرِيمِ
( 6 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 6 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 6](style/islamic/icons/mp3.png)
Ewe mwanaadamu! Nini kilicho kughuri ukamwacha Mola wako Mlezi Mtukufu?
الَّذِي خَلَقَكَ فَسَوَّاكَ فَعَدَلَكَ
( 7 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 7 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 7](style/islamic/icons/mp3.png)
Aliye kuumba, akakuweka sawa, akakunyoosha,
فِي أَيِّ صُورَةٍ مَّا شَاءَ رَكَّبَكَ
( 8 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 8 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 8](style/islamic/icons/mp3.png)
Katika sura yoyote aliyo ipenda akakujenga.
كَلَّا بَلْ تُكَذِّبُونَ بِالدِّينِ
( 9 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 9 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 9](style/islamic/icons/mp3.png)
Sivyo hivyo! Bali nyinyi mnaikanusha Siku ya Malipo.
وَإِنَّ عَلَيْكُمْ لَحَافِظِينَ
( 10 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 10 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 10](style/islamic/icons/mp3.png)
Na hakika bila ya shaka wapo walinzi juu yenu,
كِرَامًا كَاتِبِينَ
( 11 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 11 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 11](style/islamic/icons/mp3.png)
Waandishi wenye hishima,
يَعْلَمُونَ مَا تَفْعَلُونَ
( 12 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 12 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 12](style/islamic/icons/mp3.png)
Wanayajua mnayo yatenda.
إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ
( 13 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 13 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 13](style/islamic/icons/mp3.png)
Hakika wema bila ya shaka watakuwa katika neema,
وَإِنَّ الْفُجَّارَ لَفِي جَحِيمٍ
( 14 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 14 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 14](style/islamic/icons/mp3.png)
Na hakika waovu bila ya shaka watakuwa Motoni;
يَصْلَوْنَهَا يَوْمَ الدِّينِ
( 15 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 15 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 15](style/islamic/icons/mp3.png)
Wataingia humo Siku ya Malipo.
وَمَا هُمْ عَنْهَا بِغَائِبِينَ
( 16 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 16 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 16](style/islamic/icons/mp3.png)
Na hawatoacha kuwamo humo.
وَمَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ
( 17 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 17 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 17](style/islamic/icons/mp3.png)
Na nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
ثُمَّ مَا أَدْرَاكَ مَا يَوْمُ الدِّينِ
( 18 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 18 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 18](style/islamic/icons/mp3.png)
Tena nini kitakacho kujuulisha Siku ya Malipo ni siku gani?
يَوْمَ لَا تَمْلِكُ نَفْسٌ لِّنَفْسٍ شَيْئًا ۖ وَالْأَمْرُ يَوْمَئِذٍ لِّلَّهِ
( 19 ) ![Swahili - Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 19 Al-Infitar ( The Cleaving ) - Aya 19](style/islamic/icons/mp3.png)
Siku ambayo nafsi haitakuwa na madaraka yoyote juu ya nafsi; na amri yote siku hiyo ni ya Mwenyezi Mungu tu.